Tuanze Na Lyrics Kabla Ya Link … ‘ Siri Ya Mchezo ‘ Ya Rapper Fid Q …
Leo tulipaswa kukutana na season mpya ya Fidstyle Friday lakini badala yake … CEO wa Cheusidawa ameamua kutupa ile #SiriYaMchezo mzima …Siri Ya Mchezo ndio jina la ngoma mpya toka kwa #ToRe ya Top of Rap’s Elite a k a Fareed Kubanda A.K.A Fid Q … ndani ya ngoma hii Fid Q ameonyesha uwezo wa juu kabisa kiuandishi kiasi cha kuacha gumzo mitandaoni baada ya kuitambulisha ngoma yake ndani ya xxl kwa dakika kumi leo mjengoni
.
Ngoma hiyo amemshirikishwa gwiji kutoka maandishi matatu yaani TMK, Alwatan Juma Nature a k a RAMBO ambaye amekitendea haki kiitikio kwa sauti yake tuliyoimiss kwa muda mrefu.
Uongozi mzima wa Cheusidawa umeonelea ni vyema kutanguliza Lyrics za ngoma hii ambayo link yake inasubiriwa kwa hamu na watu wote (ukiwemo wewe unayesoma habari hii hivi sasa) ili mpate kuikariri mapema kabla hamjasikia jinsi Fid Q alivyoichakaza juu ya beat …
Siri Ya Mchezo
Nilipotoka mbali na ninaheshimu
nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya Biko/
Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../ sikuamini kama
nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae
kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/ Usmati
anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati
ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/
na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama
Kubanda eti unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana kwenye chati
haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa
SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya
BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../ najiuliza
tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na
wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni
jirani/
‘’ Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na
serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/
kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/Unafanya
vijana wanaumia../ Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass
ya bia..
CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2
VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA
ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang’ara ujue
kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya
uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo
leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘
wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “
saa zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘’na gari
bovu..’’ halisukumwi kwa kukaa ndani yake/ MAENDELEO ni ile
ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni kuuota au
kujiunguza? / hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/
CIVILIZATION imeadvance sasa
wanatuua economically../ hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko
free/ Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/ kila ganda litakutoa
machozi na utabaki macho juu/Ukishafika kwenye kiini niambie nini
utagundua..? zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
No comments:
Post a Comment