Monday, December 30, 2013

Mrisho Mpoto azindua Studio yake 'Waite' na wimbo mpya, kuanza kusaidia wasanii wachanga 15

rap stars


Mrisho Mpoto aka Mjomba, jana (December 29) amezindua rasmi studio yake binafsi aliyoipa jina la Waite, ambayo itakuwa ikiwasaidia wasanii wachanga.
Katika uzinduzi huo, Mrisho Mpoto alitoa vyeti maalum kwa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na 100.5 Times Fm kama sehemu ya shukurani kwa sapoti aliyopewa tangu mwanzo.
Akiongea na Tovuti ya Times Fm, Mpoto ambaye ameachia pia wimbo wake unaoitwa ‘Waite aliomshirikisha msanii ambaye hajulikani sana lakini mkali, Jerry Kano, Mpoto amesema kuwa moja kati ya project zitakazoanza kufanyiwa kazi ni pamoja na kuwasaka wasanii wachanga wenye vipaji vya kuimba ili aweze kuwasaidia pia wafike alipofikia.
“Unajua sisi hatukutokea tu tukawa hivi, walitokea watu wakatusaidia. Kwa hiyo hao vijana pia kuna watu wanatakiwa wakutane nao ambao hao watu ni sisi. Hicho kidogo tulichokipata ni ziada kabisa, tumefanikiwa na tunamaisha yetu mazuri, kwa hiyo ni sehemu ya faida niliyoipata mimi katika maisha yangu.” Amesema Mpoto.
Amesema bado hajajua moja kwa moja njia atakayoitumia kuwapata wasanii hao wachanga, lakini hatachagua aina ya muziki wanayofanya.
“Nataka atleast nianze na vijana 15 ambao naamini kwamba ntaweza kuwamanage kwa sasa kutokana na gharama, sijajua lakini watu gani wengine watanisaidia lakini nitatafuta. Lakini nataka atleast vijana 15 watoke kupitia mkono wangu, maximum vijana 30 lakini naona nianze kwanza na hawa 15.” Amefunguka Mrisho Mpoto

No comments:

Post a Comment