Thursday, November 14, 2013

P-FUNK APATA AJALI YA KUSHANGAZA CHOONI HABARI KAMILI NA PICHA INGIA HAPA

rap stars
LEGEND wa kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.
Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.
KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.
‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.
“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?
Chooni alipodondoka P-Funky na kupata majeruhi kichwani.
P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.
Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”

Rostam, Mengi, Dewji na Bakhresa waingia kwenye orodha ya matajiri 50 wa Afrika - 2013

rap stars



Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga, Rostam Aziz, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Said Bakhresa na mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji wameingia kwenye orodha ya Forbes ya watu 50 matajiri zaidi barani Africa.
Rostam Aziz ndiye aliyeongoza kwa Tanzania kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 na kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha hiyo.
Naye Reginald Mengi ambaye ni mmiliki wa magazeti lukuki nchini, TV na redio amekamata nafasi ya 34 huku hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kuingia kwenye orodha.
Kwenye nafasi ya 38 ya orodha hiyo, imeshangaza kuona Said Salim Bakhresa na Mohamed Dewji wakiwa sawa kwa utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.

BRAND NEW SONG:C-LOW FT BEN POL-ANY TIME

rap stars

WIZ KHALIFA FT JUICY J-THE PLAN (OFFICIAL VIDEO)

rap stars

Video: Mariah Carey anafananisha kufanya kazi na Nicki Minaj sawa na kufanya kazi na Shetani!?

Inawezekana kabisa Mariah Carey bado hajasahau beef kati yake na Nicki Minaj iliyozuka wakati wakifanya kazi pamoja kama majaji wa shindano la kuimba la ‘American Idol’ ambapo ilifikia hatua Nicki akamtishia maisha.
Katika interview aliyofanya na Hot 97 ya Marekani, Mariah Carey alionesha kuwa  hakuifurahia kabisa kazi yake na sababu kubwa ni pale alipoongezwa mtu ambaye mwanzo hakumtarajia katika timu ya majaji aliokuwa anawafahamu.
 Off course aliyeongezwa mwishoni baada ya kuchaguliwa majaji watatu ni Nicki Minaj hivyo kuifanya panel hiyo kuwa na majaji wanne.
“Kwa kweli, niliichukia, nilifikiri itakuwa ni panel ya watu watatu. Walinipa mchongo mzuri wa pesa, and I was like Okay. Randy Jackson atakuwa pale; nimemfahamu kwa muda wote. Alikuwa mpiga bass wangu. Haikuwa big deal.”Alisema Maria
“Lakini haikuwa hivyo. Ilikuwa kama kufanya kazi kila siku kuzimu na shetani.” Aliongeza Mariah na kuachia kicheko.
Mariah Carey na Nicki Minaj wote waliitema deal ya kuwa majaji wa shindano hilo baada ya kufanya msimu mmoja tu, na Jennifer Lopez alirudi kuchukua nafasi yake baada ya kuachana na shindano hilo kwa msimu mmoja.

Wednesday, November 13, 2013

Mansu-Li kuachia wimbo mpya ijumaa hii 'Usione Ukadhani', amewashirikisha Nikki Mbishi na Belle

rap stars

Mansu-Li kuachia wimbo mpya ijumaa hii

Sinza Star Mansoor Ally aka Mansu-Li ataachia wimbo mpya 'Usione Ukadhani' Ijumaa (November 15) akiwa amemshirikisha rapper wa Tamaduni Music Nikki Mbishi na mkali toka Morogoro, Belle 9. .

Wimbo huo umepikwa na kwa ushirikiano wa watayarishaji wawili wa muziki, Palla wa Tattoo Records na Mona Gangster wa Classic Sound.



BRAND NEW SONG:SALU T FT TAMMY-KOSA LAKE

rap stars