Monday, December 30, 2013

Taylor Swift ndio msanii wa Marekani aliyetoa misaada zaidi mwaka 2013

rap stars


Taylor Swift ndiye msanii wa Marekani aliyejitolea zaidi mwaka 2013, kwa mujibu wa mtandao wa  DoSomething.org.  muimbaji huyo pamoja na misaada mingine alifanya show  jijini London kusaidia vijana wasio na makazi.
Katika nafasi ya pili wapo kundi la One Direction waliokusanya zaidi ya dola milioni 3 kusaidia shirika la Uingereza la Comic Relief pamoja na kukusanya  $800,000 kusaidia utafiti wa saratani.
Hii ni orodha nzima iliyopewa jina "Top 20 Celebs Gone Good":
1. Taylor Swift
2. One Direction
3. Beyoncé
4. Paul Walker
5. Macklemore & Ryan Lewis
6. Sandra Bullock
7. Kerry Washington
8. Ian Somerhalder
9. Ryan Seacrest
10. Carrie Underwood
11. Jennifer Lawrence
12. Alicia Keys
13. Bryan Cranston and Aaron Paul
14. Miley Cyrus
15. Demi Lovato
16. Blake Shelton
17. Mindy Kaling
18. Kevin Durant
19. Kendrick Lamar
20. Justin Bieber

Mrisho Mpoto azindua Studio yake 'Waite' na wimbo mpya, kuanza kusaidia wasanii wachanga 15

rap stars


Mrisho Mpoto aka Mjomba, jana (December 29) amezindua rasmi studio yake binafsi aliyoipa jina la Waite, ambayo itakuwa ikiwasaidia wasanii wachanga.
Katika uzinduzi huo, Mrisho Mpoto alitoa vyeti maalum kwa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na 100.5 Times Fm kama sehemu ya shukurani kwa sapoti aliyopewa tangu mwanzo.
Akiongea na Tovuti ya Times Fm, Mpoto ambaye ameachia pia wimbo wake unaoitwa ‘Waite aliomshirikisha msanii ambaye hajulikani sana lakini mkali, Jerry Kano, Mpoto amesema kuwa moja kati ya project zitakazoanza kufanyiwa kazi ni pamoja na kuwasaka wasanii wachanga wenye vipaji vya kuimba ili aweze kuwasaidia pia wafike alipofikia.
“Unajua sisi hatukutokea tu tukawa hivi, walitokea watu wakatusaidia. Kwa hiyo hao vijana pia kuna watu wanatakiwa wakutane nao ambao hao watu ni sisi. Hicho kidogo tulichokipata ni ziada kabisa, tumefanikiwa na tunamaisha yetu mazuri, kwa hiyo ni sehemu ya faida niliyoipata mimi katika maisha yangu.” Amesema Mpoto.
Amesema bado hajajua moja kwa moja njia atakayoitumia kuwapata wasanii hao wachanga, lakini hatachagua aina ya muziki wanayofanya.
“Nataka atleast nianze na vijana 15 ambao naamini kwamba ntaweza kuwamanage kwa sasa kutokana na gharama, sijajua lakini watu gani wengine watanisaidia lakini nitatafuta. Lakini nataka atleast vijana 15 watoke kupitia mkono wangu, maximum vijana 30 lakini naona nianze kwanza na hawa 15.” Amefunguka Mrisho Mpoto

Wednesday, December 11, 2013

TUNAPENDA KUWATANGAZIA MABADILIKO YA TAREHE YA LiVE HiP HOP II KUWA ITAFANYIKA TAREHE 28|12|2013 PALE PALE NYUMBANI LOUNGE.

rap stars

Mona Gangster awakutanisha Belle 9, Steve RnB, Ben Pol, Nuruel, Stereo, Young Killer kwenye project ya kupinga dawa za kulevya

rap stars


Producer wa studio za Classic Sound, Mona Gangster amewakutanisha wakali kadhaa wa hip hop na R&B hapa Tanzania kwa lengo la kusaidia kufikisha ujumbe wa kupinga matumizi na biashara ya madawa ya kulevya nchini.
Mona G ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa  ameamua kufanya project hiyo ili kusaidia kupiga vita na kuhamasisha vijana hasa wasanii kuacha kutumia mihadarati.
Amesema ameamua kuwatumia wasanii wakubwa ambao watafanya nyimbo kadhaa za pamoja zenye ujumbe wa aiana hiyo, na kwamba tayari wameshafanya wimbo mmoja alioupa jina ‘Usikate Tamaa’, na humo ndani wameshirikishwa Ben Pol, Belle 9, Steve RnB,Bright, Nuruel, Young Killer na Stereo.
“Sijaiachia bado, kwa sababu tulifanya hadi video lakini bado video pia haijatoka. Naangalia target ni jinsi gani naweza kupush huo wimbo kwa sababu lengo sio kuachia tu wimbo. Lengo ni kwamba tuweze kupata hata sponsorship na tufikishe ujumbe kwa kila mtanzania na sio tu hapa Dar es Salaam, ila tuweze kufikisha hata mkoa kwa mkoa, kwa hiyo ni kitu ambacho kinahitaji maandalizi.” Amesema Mona Gangaster.
 Kuhusu lini ngoma hiyo itaachiwa rasmi, Mona G alifunguka, “Siwezi kuachia tu kama nyimbo nyingine zinavyoachiwa, hii ni project so kuna vitu naviwekaweka sawa then ntairelease.”

Mixtape ya Wakazi 'MYU: The Trinity Mixtape (UTATU MTAKATIFU)' yaingia sokoni

rap stars


Mixtape ya Wakazi iitwayo, MYU: The Trinity Mixtape (UTATU MTAKATIFU) Imeingia sokoni rasmi.
Mixtape hiyo ni mkusanyiko wa mixtape zake tatu za MYU.
Kupitia Instagram Wakazi ameandika:
MYU: The Trinity Mixtape (UTATU MTAKATIFU) is now available in the streets of Dar Es salaam for Tsh. 5000/= only. Go to Msasani Club (KILINGENI), Nyumbani Lounge, Diplomatic barbershop (Mbezi), B'ball Kitaa (Spiders), Kenton High School Mwenge (Tomorrow), Nyama Choma Festival (Postal Grounds) or Call Wakazi (+255768367673) for your copy!! The Mixtape will also be available online exclusively at SPINLET @Sniplet (www.spinlet.com). You can download the spinlet app on your android or iPhone for better experience.”