Producer wa studio za Classic Sound, Mona Gangster
amewakutanisha wakali kadhaa wa hip hop na R&B hapa Tanzania kwa
lengo la kusaidia kufikisha ujumbe wa kupinga matumizi na biashara ya
madawa ya kulevya nchini.
Mona G ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa ameamua kufanya project
hiyo ili kusaidia kupiga vita na kuhamasisha vijana hasa wasanii kuacha
kutumia mihadarati.
Amesema ameamua kuwatumia wasanii wakubwa ambao watafanya nyimbo kadhaa za pamoja zenye ujumbe wa aiana hiyo, na kwamba tayari wameshafanya wimbo mmoja alioupa jina ‘Usikate Tamaa’, na humo ndani wameshirikishwa Ben Pol, Belle 9, Steve RnB,Bright, Nuruel, Young Killer na Stereo.
“Sijaiachia bado, kwa sababu tulifanya hadi video lakini bado video pia haijatoka. Naangalia target ni jinsi gani naweza kupush huo wimbo kwa sababu lengo sio kuachia tu wimbo. Lengo ni kwamba tuweze kupata hata sponsorship na tufikishe ujumbe kwa kila mtanzania na sio tu hapa Dar es Salaam, ila tuweze kufikisha hata mkoa kwa mkoa, kwa hiyo ni kitu ambacho kinahitaji maandalizi.” Amesema Mona Gangaster.
Kuhusu lini ngoma hiyo itaachiwa rasmi, Mona G alifunguka, “Siwezi kuachia tu kama nyimbo nyingine zinavyoachiwa, hii ni project so kuna vitu naviwekaweka sawa then ntairelease.”

No comments:
Post a Comment