Showing posts with label chris brown. Show all posts
Showing posts with label chris brown. Show all posts

Tuesday, October 29, 2013

Chris Brown aachiwa huru baada ya kukaa selo masaa 36, apewa masharti ya kukaa mbali na mtu aliyemjeruhi

rap stars
Chris Brown aachiwa huru baada ya kukaa selo masaa 36, apewa masharti ya kukaa mbali na mtu aliyemjeruhi

Chris Brown amenusurika kufungwa jela miaka minne kama angekutwa na hatia baada ya kushirikiana na mlinzi wake kumpiga na kumjeruhi pua mtu aliyekuwa anajaribu kumpiga picha.
Kwa mujibu wa TMZ Chris na mlinzi wake waliachiwa huru jana (October 28), baada ya jaji kupunguza ukali wa mashtaka yaliyokuwa yanamkabiri kutoka ‘Felony’ (mashtaka serious na yenye nguvu), na kuwa ‘Misdemeanor’ (mashtaka ambayo sio serious sana kama Felony).
Kupunguzwa nguvu kwa mashtaka hayo kulimpa nafasi Chris Brown kutoka selo bila kupewa masharti ya kuhudhuria tena katika kituo cha polisi wala mahakamani, na hii ni baada ya kuonekana hana hatia katika mashtaka hayo.