Kwa mujibu wa TMZ Chris na mlinzi wake waliachiwa huru jana (October 28), baada ya jaji kupunguza ukali wa mashtaka yaliyokuwa yanamkabiri kutoka ‘Felony’ (mashtaka serious na yenye nguvu), na kuwa ‘Misdemeanor’ (mashtaka ambayo sio serious sana kama Felony).
Kupunguzwa nguvu kwa mashtaka hayo kulimpa nafasi Chris Brown kutoka selo bila kupewa masharti ya kuhudhuria tena katika kituo cha polisi wala mahakamani, na hii ni baada ya kuonekana hana hatia katika mashtaka hayo.
Hata hivyo mwimbaji huyo amepewa masharti ya kukaa mbali na mtu aliyemjeruhi, umbali wa takribani mita 100.
Awali ilitolewa amri ya kumfanyia Chris vipimo vya matumizi ya dawa za kulevya, lakini Jaji alipangua uamuzi huo.
Majeruhi wa tukio hilo ameelezea kuwa Chris na mlinzi wake walishirikiana kumshambulia ambapo mlinzi huyo alimpiga ngumi, kisha Chris brown akaendelea kupiga kelele na kusapoti huku akitoa matusi.
Hata hivyo watu wa karibu wa Chris Brown wameeleza kuwa mtu huyo alikuwa analazimisha kuingia kwenye tour bus ya Chris, maelezo ambayo yalipingwa na mtu huyo ambae anadai kuwa alikuwa anampiga picha Chris aliyekuwa anapiga picha na wasichana nje ya hotel.
Polisi wamesema mwanaume aliyeshambuliwa bado anaendelea na matibabu ya pua yake.
No comments:
Post a Comment