Friday, November 8, 2013

ILLMATIX PACHA ONE & SONGA LIVE HiP HOP ON TAREHE 30|11|2013 SIO YA KUKOSA

rap stars

 The fusion night Kutoka tamaduni muziki wanajulikana kama illmatix pacha one & songa wakiwa pamoja na kad go, dizasta na balle watafanya live show yakufa mtu ndani ya viwanja vya nyumbani lounge siku ya tarehe 30/11/2013 kwa wadau wa hip hop na hasa  wapenzi wa tamaduni muzik hii sio yakukosa

Audio:Busta Rhymes aachia 'Thank You' aliyomshirikisha Kanye West, Lil Wayne na Q-Tip

rap stars
Baada ya ile subira ya muda mrefu, hatimaye rapper mkongwe Busta Rhymes ambaye kwa sasa anawakilisha Cash Money ameachia ngoma yake mpya ‘Thank You’ ambayo itapatikana kwenye album yake ya Extinction Level Event 2.
Busta amewashirikisha Lil Wayne, Kanye West na Q-Tip kuhakikisha kinatoka kitu kizito.
Isikilize hapa, ni explicit version.

Tuesday, November 5, 2013

Makala: Video ya 'Touch' ya Wakazi itaongeza idadi ya video za Tanzania zinazooneshwa na Channel kubwa za Kimataifa



‘Kizuri ni kizuri , lakini chenye ubora ni bora’, naomba niutumie mstari huu wa Fid Q kabla sijaendelea na kile nachotaka kukiandika kwa ufupi kwa kuwa mstari huo ndio ulionijia kichwani wakati naiangalia video ya wimbo wa Wakazi ‘Touch’.
Zipo video nyingi nzuri lakini pia zipo video ‘bora’, hapa namaanisha ubora umebeba uzuri plus vitu vingine ambavyo ni vya kiuweledi na ubunifu.
Naweza kusema video ya ‘Wakazi ni kati ya video bora za Tanzania ambazo nina uhakika zitavuka border bila shida.
Sio kwa sababu imefanywa na kampuni ya nje ya Planet Image, la hasha, lakini ni kwa jinsi ambavyo haiko complicated, shots zimepigwa vizuri sana na ziko clear, na mchanganyaji wa picha ameweza kuifanya isichoshe macho na kwenda vizuri na midondoko ya midundo.

Mimi kama mtazamaji wa kawaida tu hivyo vimenivutia hata zaidi ya complicationi za kuweka shots za sehemu nyingi na kupoteza mtiriko..ni uandishi simple wa script unaofikisha kitu katika ubora.
Nimependa pia selection ya picha zilizochukuliwa ambazo hazileti ukakasi kuangalia japokuwa ujumbe wa wimbo ulikuwa umekaa katika hali ambayo labda muongozaji mwingine angeweza kuifanya iwe na hali fulani ya muonekano wa mahaba mengi hivi, lakini ameipeleka club hivi sehemu ambayo ngoma inabang zaidi.
Lakini hata kilichooneshwa huko kimekuwa fair hasa kwakuzingatia watazamaji wa hapa bongo wanaoangalia na baadhi familia sebuleni.
Wakazi aka Swag Bovu pia amecheza kama mzoefu wa muda mrefu kwenye lens za camera.
Japokuwa zipo changamoto lakini naamini zitakuwa chache sana kuliko kazi nzuri iliyofanyika.

Naamini hii video itaiongezea nguvu zaidi audio ya wimbo huu ambao ulifanywa na kampuni ya Clinton X (Afrika kusini) na kuguswa pia na mtanzania ‘Lucci’, audio ambayo inafanya vizuri kwenye chart za muziki hapa nyumbani na baadhi ya sehemu barani Afrika.

Itawakumbusha wengi pia kile alichokifanya kwenye jukwaa la BBA The Chase July mwaka huu pale alipouimba wimbo huu na kufunika japo alikuwa msanii mpya pia hasa kwa baadhi ya wabongo ambao walimfahamu kupitia jukwaa hilo, huku wale ambao wanaujua uwezo wake wakiona amefanya kile walichotegemea.
Kwa ufupi, naamini itachukua siku chache kabla hatujaiona video ya 'Touch' kwenye channels kama MTV, Channel O, Trace na nyingine na kuongeza idadi ya video chache za wabongo zinazobang kwenye vituo hivyo.
Ad space


Friday, November 1, 2013

OFFICIAL VIDEO BY ROMA FT STORY-2013

Angalia video mpya ya wimbo wa Roma Mkatoliki '2030', iliyofanya na kampuni ya Nisher Entertainment na kuongezwa na 'Nisher'.

rap stars

Geez Mabovu:Wasanii wengi wanatumia dawa za kulevya kwa kuiga na sio kwa sababu ya stress za game

rap stars

Kama unakumbuka ile kauli ya Dudu Baya kwamba wasanii wengi wanajihusisha na uvutaji bangi na kubwia unga kwasababu ya stress za game,sasa ‘Mtoto wa Kiume’ Geez Mabovu ameipinga kauli hiyo na kusema kwamba wasanii hutumia dawa za kulevya kwa kuiga na sio stress.
Geez Mabovu ambaye hivi Karibu aliachia wimbo mpya ‘Hip Hop Msingi’ unaoelezea masuala ya Hip Hop kwa ujumla,amewaasa wasanii wenzake kutokata tamaa mapema na kuanza kulalamika kwamba unga ndio chanzo cha matatizo.
Geez amefunguka kupitia tovuti ya Times fm,wakati anatoa maoni ya mabadiliko ya tabia kwa wasanii.
"Wasanii wengi wanabwia unga kwa kuwaiga wasanii wa kimarekani kama wakina Lil Wayne wale wenzetu wana mkwanja,lakini wasanii wetu wanadai stress za game ndio zinawafanya wabwie unga,mimi nadhani umefika  wakati wasanii kujitambua na kuachana na lawama,tujitambua na tuchape kazi lakini habari za kusema kwamba kubwia unga kunatokana na stress za game si kweli." Amesema Mabovu.
Katika mazungumzo hayo pia Geez  Mabovu amesema alishawahi kuvuta bangi takriban miaka 8 lakini kwa sasa ameacha.
‘Mimi niliwahi kuvuta Bangi takribani miaka 8 iliyopita na wala sikupatwa na matatizo yoyote mpaka sasa niko zangu fresh na life inasonga’

Rick Ross aurudia wimbo wa B.I.G 'You're Nobody Until Somebody Kills You', kushambuliwa kwa risasi ni chanzo cha idea yake

rap stars

Big boss wa MMG, William Roberts II aka Rick Ross ameamua kuirudia ngoma ya marehemu Notorious B.I.G ‘You’re Nobody (Until Somebody Kills You)’, moja kati ya nyimbo zilizokuwa katika album ya B.I.G ‘Life After Death’ ambapo aligusia kuhusu kifo chake.
Rick Ross amei-sample ngoma hiyo na kuiweka kwenye album yake ‘Mastermind’ inayotarajiwa kutoka rasmi December 17 mwaka huu.
Hivi karibuni Rozay aliwaalika studio baadhi ya bloggers na wataalam wa muziki na akawasikilizisha baadhi ya nyimbo zitakazokuwemo kwenye album hiyo.
Kwa mujibu wa mhariri wa Vibe, John Kennedy ngoma hiyo aliyoisample Rick Ross ilivuta usikivu zaidi, na kwamba katika ngoma hiyo anasikika akisema kuwa anahisi Biggie angeweza kuhusika na ngoma hiyo, kisha inasikika sauti ikiripoti kuhusu Rick Ross kushambuliwa kwa risasi January mwaka huu.
Baada ya hapo unadondoka mdundo wa wimbo wa Biggie ‘You’re Nobody (Until Somebody Kills You)’ na Rick Ross anaanza kuelezea kuhusu jaribio la kuuawa huku sauti yake ikiwa imewekewa effect inasikika kwa mbali kama ya Biggie.
Biggie aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari akiwa amekaa kwenye siti ya abiria mwaka 1997, jijini Los Angeles.