Kama unakumbuka ile kauli ya Dudu Baya kwamba wasanii wengi wanajihusisha na uvutaji bangi na kubwia unga kwasababu ya stress za game,sasa ‘Mtoto wa Kiume’ Geez Mabovu ameipinga kauli hiyo na kusema kwamba wasanii hutumia dawa za kulevya kwa kuiga na sio stress.
Geez Mabovu ambaye hivi Karibu aliachia wimbo mpya ‘Hip Hop Msingi’ unaoelezea masuala ya Hip Hop kwa ujumla,amewaasa wasanii wenzake kutokata tamaa mapema na kuanza kulalamika kwamba unga ndio chanzo cha matatizo.
Geez amefunguka kupitia tovuti ya Times fm,wakati anatoa maoni ya mabadiliko ya tabia kwa wasanii.
"Wasanii wengi wanabwia unga kwa kuwaiga wasanii wa kimarekani kama wakina Lil Wayne wale wenzetu wana mkwanja,lakini wasanii wetu wanadai stress za game ndio zinawafanya wabwie unga,mimi nadhani umefika wakati wasanii kujitambua na kuachana na lawama,tujitambua na tuchape kazi lakini habari za kusema kwamba kubwia unga kunatokana na stress za game si kweli." Amesema Mabovu.
Katika mazungumzo hayo pia Geez Mabovu amesema alishawahi kuvuta bangi takriban miaka 8 lakini kwa sasa ameacha.
‘Mimi niliwahi kuvuta Bangi takribani miaka 8 iliyopita na wala sikupatwa na matatizo yoyote mpaka sasa niko zangu fresh na life inasonga’
No comments:
Post a Comment