Saturday, November 23, 2013

Uongozi wa B'Hits kutoa maelezo ya kina kupitia Bongo Dot Home ya 100.5 Times fm kuhusu kuondolewa kwa Vanessa, Gosby, Mabeste na wote waliowahi kupita

rap stars

Uongozi wa B’Hitz Music Group umeamua kuzungumza kwa kina kuhusu sakata la kuwaondoa wasanii watatu walioukuwa chini ya studio hiyo ambao ni Mabeste, Vanessa, na Gosby.
Uongozi huo utasikika exclusively kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times fm leo (November 23) kuanzia saa kumi kamili jioni.
Akiongea na tovuti ya Times fm, mtangazaji wa kipindi hicho Jabir Saleh aka Kuvichaka amesema pamoja na mambo mengine, uongozi huo utazungumzia kuhusu malalamiko ya Mabeste kuwa amedhalilishwa na C.E.O wa B’Hits Hermy B.
Amesema kuwa uongozi huo pia utatoa ufafanuzi wa kina kuhusu wasanii wote waliowahi kufanya kazi chini ya label hiyo na kuondoka ili kutoa picha halisi ya mambo yalivyokuwa.
Bongo Dot Home inakuwa hewani kila jumamosi saa kumi kamili jioni hadi saa moja usiku, na kuendeshwa na Jabir Saleh, Moko Biashara (One B), na Dj K_U
Unaweza kusikiliza live online, bofya hapa http://bit.ly/HHnfKt

Mr. Blue anatafutwa na polisi wa Kenya kwa utapeli

rap stars



Hitmaker wa ‘Mapozi’ Mr. Blue aka Kabayser anatafutwa na polisi wa Kenya. Msanii huyo anatafutwa kwa shutuma za kushindwa kutokea kwenye show aliyokuwa amesaini mkataba huko Mombasa, Kenya. Mr. Blue alikuwa anatakiwa kutumbuiza kwenye maeneo ya Office Restaurant, Likoni na Mariakani Jubilant Hotel, November 16 na 17.
Mratibu wa show hiyo, Sammy Ondwar Onyango, aliamua kwenda kushtaki polisi sababu anadai alikuwa ameshamlipa msanii huyo sehemu ya malipo waliyokuwa wamekubaliana.
“Mr Blue si mtu mwaminifu kabisa. Aliwahi kuniangusha pia mwaka 2012 kwenye show ya Jet Bar, Likoni, baada ya kudai kuwa alikosa basi ya kwenda Mombasa na nililazimika kuingia zaidi mfukoni kumlipia basi jingine,” Onyango aliliambia gazeti la The Star.
Promota huyo amesema kwenye tukio la sasa, walikubaliana kumlipa shilingi 100,000 (za Kenya) ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.8  na tayari alikuwa ameshamlipa shilingi 40,000 kupitia M-Pesa.
Kesi hiyo imeripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Likoni.
Gazeti hilo limesema baada ya kuwasiliana na Mr Blue kwa simu, aliweza kujibu kwa ujumbe mfupi wa simu kwamba alikuwa akiendesha gari na simu haikupatikana tena.

Tuesday, November 19, 2013

BRAND NEW TRACK:DARASA FT MCHIZI MOX & SHILOLE-MIKONO JUU

rap stars
Kwa muda mrefu hapa Tanzania kumekuwa na kutoeleweka ama wengine husema kwa ufupi tu kuwa haiwezekani kuchanganya muziki wa Taarabu/Mduara na hop hop na kwamba mchanganyiko huo hauwezekani.
Hizo hisia hazikuwa tatizo kwa rapper Darasa aliyechukua uamuzi wa kumpa shavu Shilole kwenye ngoma yake ‘Mikono Juu’ inayopatikana kwenye mixtape yake ya ‘Dream Big Chapakazi’, mchanganyiko ambao umetengeneza ngoma kali.
Lakini kumbe rapper huyo alifanya hivyo tu kwa kuwa aliona sio lazima kila siku kuwa serious kwa hiyo akaamua kutania tu kwa kumpa shavu ShiShi atupie melody za mduara kwa mbali kwenye ngoma hiyo.
Darasa amefunguka kwenye kipindi cha ‘The Jump Off’ cha 100.5 Times fm alipokuwa akiutambulisha wimbo wake, ambapo Jabir Saleh aka Kuvichaka alitaka kufahamu ngoma hiyo ni aina gani ya hip hop.
“Kwenye maisha hauwezi kuwa serious muda wote, sasa huu ndio muda wangu wa kutania na ndio maana nacheza na ndio maana nimeweka kwenye mixtape. Nikiwa serious narudi darasani na tunafanya mambo yetu yale.” Alifunguka Darasa.
Alipoulizwa kuhusu lengo lake la kuwakutanisha Shilole kwenye ngoma hiy, mkali huyo wa ‘Weka Ngoma’ alifunguka, “Nilikuwa nataka tofauti, as you can see umeona tofauti. Na tofauti niliyokuwa mimi, kwanza nilikuwa nachukua mashabiki wa Shilole na mashabiki wangu nawaweka kwenye chumba kimoja.
 “Tunatengeneza familia kutoka kwa watu ambao tulikuwa hatufahamiani tunakaa chumba kimoja, marafiki wangu mimi na marafiki wa Shilole na Mchizi Mox sasa hivi wamekaa chumba kimoja wanatusikiliza.” Darasa alifafanua.

Thursday, November 14, 2013

Exclusive: Linex kusaini mkataba na kampuni itakayosimamia muziki na ratiba ya maisha yake binafsi, 'sitaki u-manager wa kuombana hela'

rap stars



Mwimbaji wa ‘Kimugina’ Linex anatarajia kusaini mkataba na kampuni inayoendeshwa na vijana wa hapa Tanzania itakayosimamia kazi zake za muziki, lakini tofauti na management nyingi za Kibongo kampuni hiyo itasimamia hadi ratiba zake binafsi ikiwa ni pamoja na mitoko ya kawaida.

Linex ameiambia tovuti ya Times fm kuwa kwa muda wa miaka minne amekuwa akifanya kazi bila kuwa chini ya management yoyote kwa kuwa alikuwa hajapata manager anaemfaa.

P-FUNK APATA AJALI YA KUSHANGAZA CHOONI HABARI KAMILI NA PICHA INGIA HAPA

rap stars
LEGEND wa kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.
Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.
KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.
‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.
“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?
Chooni alipodondoka P-Funky na kupata majeruhi kichwani.
P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.
Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”

Rostam, Mengi, Dewji na Bakhresa waingia kwenye orodha ya matajiri 50 wa Afrika - 2013

rap stars



Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga, Rostam Aziz, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Said Bakhresa na mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji wameingia kwenye orodha ya Forbes ya watu 50 matajiri zaidi barani Africa.
Rostam Aziz ndiye aliyeongoza kwa Tanzania kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 na kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha hiyo.
Naye Reginald Mengi ambaye ni mmiliki wa magazeti lukuki nchini, TV na redio amekamata nafasi ya 34 huku hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kuingia kwenye orodha.
Kwenye nafasi ya 38 ya orodha hiyo, imeshangaza kuona Said Salim Bakhresa na Mohamed Dewji wakiwa sawa kwa utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.

BRAND NEW SONG:C-LOW FT BEN POL-ANY TIME

rap stars

WIZ KHALIFA FT JUICY J-THE PLAN (OFFICIAL VIDEO)

rap stars

Video: Mariah Carey anafananisha kufanya kazi na Nicki Minaj sawa na kufanya kazi na Shetani!?

Inawezekana kabisa Mariah Carey bado hajasahau beef kati yake na Nicki Minaj iliyozuka wakati wakifanya kazi pamoja kama majaji wa shindano la kuimba la ‘American Idol’ ambapo ilifikia hatua Nicki akamtishia maisha.
Katika interview aliyofanya na Hot 97 ya Marekani, Mariah Carey alionesha kuwa  hakuifurahia kabisa kazi yake na sababu kubwa ni pale alipoongezwa mtu ambaye mwanzo hakumtarajia katika timu ya majaji aliokuwa anawafahamu.
 Off course aliyeongezwa mwishoni baada ya kuchaguliwa majaji watatu ni Nicki Minaj hivyo kuifanya panel hiyo kuwa na majaji wanne.
“Kwa kweli, niliichukia, nilifikiri itakuwa ni panel ya watu watatu. Walinipa mchongo mzuri wa pesa, and I was like Okay. Randy Jackson atakuwa pale; nimemfahamu kwa muda wote. Alikuwa mpiga bass wangu. Haikuwa big deal.”Alisema Maria
“Lakini haikuwa hivyo. Ilikuwa kama kufanya kazi kila siku kuzimu na shetani.” Aliongeza Mariah na kuachia kicheko.
Mariah Carey na Nicki Minaj wote waliitema deal ya kuwa majaji wa shindano hilo baada ya kufanya msimu mmoja tu, na Jennifer Lopez alirudi kuchukua nafasi yake baada ya kuachana na shindano hilo kwa msimu mmoja.

Wednesday, November 13, 2013

Mansu-Li kuachia wimbo mpya ijumaa hii 'Usione Ukadhani', amewashirikisha Nikki Mbishi na Belle

rap stars

Mansu-Li kuachia wimbo mpya ijumaa hii

Sinza Star Mansoor Ally aka Mansu-Li ataachia wimbo mpya 'Usione Ukadhani' Ijumaa (November 15) akiwa amemshirikisha rapper wa Tamaduni Music Nikki Mbishi na mkali toka Morogoro, Belle 9. .

Wimbo huo umepikwa na kwa ushirikiano wa watayarishaji wawili wa muziki, Palla wa Tattoo Records na Mona Gangster wa Classic Sound.



BRAND NEW SONG:SALU T FT TAMMY-KOSA LAKE

rap stars

Friday, November 8, 2013

ILLMATIX PACHA ONE & SONGA LIVE HiP HOP ON TAREHE 30|11|2013 SIO YA KUKOSA

rap stars

 The fusion night Kutoka tamaduni muziki wanajulikana kama illmatix pacha one & songa wakiwa pamoja na kad go, dizasta na balle watafanya live show yakufa mtu ndani ya viwanja vya nyumbani lounge siku ya tarehe 30/11/2013 kwa wadau wa hip hop na hasa  wapenzi wa tamaduni muzik hii sio yakukosa

Audio:Busta Rhymes aachia 'Thank You' aliyomshirikisha Kanye West, Lil Wayne na Q-Tip

rap stars
Baada ya ile subira ya muda mrefu, hatimaye rapper mkongwe Busta Rhymes ambaye kwa sasa anawakilisha Cash Money ameachia ngoma yake mpya ‘Thank You’ ambayo itapatikana kwenye album yake ya Extinction Level Event 2.
Busta amewashirikisha Lil Wayne, Kanye West na Q-Tip kuhakikisha kinatoka kitu kizito.
Isikilize hapa, ni explicit version.

Tuesday, November 5, 2013

Makala: Video ya 'Touch' ya Wakazi itaongeza idadi ya video za Tanzania zinazooneshwa na Channel kubwa za Kimataifa



‘Kizuri ni kizuri , lakini chenye ubora ni bora’, naomba niutumie mstari huu wa Fid Q kabla sijaendelea na kile nachotaka kukiandika kwa ufupi kwa kuwa mstari huo ndio ulionijia kichwani wakati naiangalia video ya wimbo wa Wakazi ‘Touch’.
Zipo video nyingi nzuri lakini pia zipo video ‘bora’, hapa namaanisha ubora umebeba uzuri plus vitu vingine ambavyo ni vya kiuweledi na ubunifu.
Naweza kusema video ya ‘Wakazi ni kati ya video bora za Tanzania ambazo nina uhakika zitavuka border bila shida.
Sio kwa sababu imefanywa na kampuni ya nje ya Planet Image, la hasha, lakini ni kwa jinsi ambavyo haiko complicated, shots zimepigwa vizuri sana na ziko clear, na mchanganyaji wa picha ameweza kuifanya isichoshe macho na kwenda vizuri na midondoko ya midundo.

Mimi kama mtazamaji wa kawaida tu hivyo vimenivutia hata zaidi ya complicationi za kuweka shots za sehemu nyingi na kupoteza mtiriko..ni uandishi simple wa script unaofikisha kitu katika ubora.
Nimependa pia selection ya picha zilizochukuliwa ambazo hazileti ukakasi kuangalia japokuwa ujumbe wa wimbo ulikuwa umekaa katika hali ambayo labda muongozaji mwingine angeweza kuifanya iwe na hali fulani ya muonekano wa mahaba mengi hivi, lakini ameipeleka club hivi sehemu ambayo ngoma inabang zaidi.
Lakini hata kilichooneshwa huko kimekuwa fair hasa kwakuzingatia watazamaji wa hapa bongo wanaoangalia na baadhi familia sebuleni.
Wakazi aka Swag Bovu pia amecheza kama mzoefu wa muda mrefu kwenye lens za camera.
Japokuwa zipo changamoto lakini naamini zitakuwa chache sana kuliko kazi nzuri iliyofanyika.

Naamini hii video itaiongezea nguvu zaidi audio ya wimbo huu ambao ulifanywa na kampuni ya Clinton X (Afrika kusini) na kuguswa pia na mtanzania ‘Lucci’, audio ambayo inafanya vizuri kwenye chart za muziki hapa nyumbani na baadhi ya sehemu barani Afrika.

Itawakumbusha wengi pia kile alichokifanya kwenye jukwaa la BBA The Chase July mwaka huu pale alipouimba wimbo huu na kufunika japo alikuwa msanii mpya pia hasa kwa baadhi ya wabongo ambao walimfahamu kupitia jukwaa hilo, huku wale ambao wanaujua uwezo wake wakiona amefanya kile walichotegemea.
Kwa ufupi, naamini itachukua siku chache kabla hatujaiona video ya 'Touch' kwenye channels kama MTV, Channel O, Trace na nyingine na kuongeza idadi ya video chache za wabongo zinazobang kwenye vituo hivyo.
Ad space


Friday, November 1, 2013

OFFICIAL VIDEO BY ROMA FT STORY-2013

Angalia video mpya ya wimbo wa Roma Mkatoliki '2030', iliyofanya na kampuni ya Nisher Entertainment na kuongezwa na 'Nisher'.

rap stars

Geez Mabovu:Wasanii wengi wanatumia dawa za kulevya kwa kuiga na sio kwa sababu ya stress za game

rap stars

Kama unakumbuka ile kauli ya Dudu Baya kwamba wasanii wengi wanajihusisha na uvutaji bangi na kubwia unga kwasababu ya stress za game,sasa ‘Mtoto wa Kiume’ Geez Mabovu ameipinga kauli hiyo na kusema kwamba wasanii hutumia dawa za kulevya kwa kuiga na sio stress.
Geez Mabovu ambaye hivi Karibu aliachia wimbo mpya ‘Hip Hop Msingi’ unaoelezea masuala ya Hip Hop kwa ujumla,amewaasa wasanii wenzake kutokata tamaa mapema na kuanza kulalamika kwamba unga ndio chanzo cha matatizo.
Geez amefunguka kupitia tovuti ya Times fm,wakati anatoa maoni ya mabadiliko ya tabia kwa wasanii.
"Wasanii wengi wanabwia unga kwa kuwaiga wasanii wa kimarekani kama wakina Lil Wayne wale wenzetu wana mkwanja,lakini wasanii wetu wanadai stress za game ndio zinawafanya wabwie unga,mimi nadhani umefika  wakati wasanii kujitambua na kuachana na lawama,tujitambua na tuchape kazi lakini habari za kusema kwamba kubwia unga kunatokana na stress za game si kweli." Amesema Mabovu.
Katika mazungumzo hayo pia Geez  Mabovu amesema alishawahi kuvuta bangi takriban miaka 8 lakini kwa sasa ameacha.
‘Mimi niliwahi kuvuta Bangi takribani miaka 8 iliyopita na wala sikupatwa na matatizo yoyote mpaka sasa niko zangu fresh na life inasonga’

Rick Ross aurudia wimbo wa B.I.G 'You're Nobody Until Somebody Kills You', kushambuliwa kwa risasi ni chanzo cha idea yake

rap stars

Big boss wa MMG, William Roberts II aka Rick Ross ameamua kuirudia ngoma ya marehemu Notorious B.I.G ‘You’re Nobody (Until Somebody Kills You)’, moja kati ya nyimbo zilizokuwa katika album ya B.I.G ‘Life After Death’ ambapo aligusia kuhusu kifo chake.
Rick Ross amei-sample ngoma hiyo na kuiweka kwenye album yake ‘Mastermind’ inayotarajiwa kutoka rasmi December 17 mwaka huu.
Hivi karibuni Rozay aliwaalika studio baadhi ya bloggers na wataalam wa muziki na akawasikilizisha baadhi ya nyimbo zitakazokuwemo kwenye album hiyo.
Kwa mujibu wa mhariri wa Vibe, John Kennedy ngoma hiyo aliyoisample Rick Ross ilivuta usikivu zaidi, na kwamba katika ngoma hiyo anasikika akisema kuwa anahisi Biggie angeweza kuhusika na ngoma hiyo, kisha inasikika sauti ikiripoti kuhusu Rick Ross kushambuliwa kwa risasi January mwaka huu.
Baada ya hapo unadondoka mdundo wa wimbo wa Biggie ‘You’re Nobody (Until Somebody Kills You)’ na Rick Ross anaanza kuelezea kuhusu jaribio la kuuawa huku sauti yake ikiwa imewekewa effect inasikika kwa mbali kama ya Biggie.
Biggie aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari akiwa amekaa kwenye siti ya abiria mwaka 1997, jijini Los Angeles.