rap stars
Kwa muda mrefu hapa Tanzania kumekuwa na kutoeleweka ama wengine
husema kwa ufupi tu kuwa haiwezekani kuchanganya muziki wa
Taarabu/Mduara na hop hop na kwamba mchanganyiko huo hauwezekani.
Hizo hisia hazikuwa tatizo kwa rapper Darasa aliyechukua uamuzi wa
kumpa shavu Shilole kwenye ngoma yake ‘Mikono Juu’ inayopatikana kwenye
mixtape yake ya ‘Dream Big Chapakazi’, mchanganyiko ambao umetengeneza
ngoma kali.
Lakini kumbe rapper huyo alifanya hivyo tu kwa kuwa aliona sio lazima
kila siku kuwa serious kwa hiyo akaamua kutania tu kwa kumpa shavu
ShiShi atupie melody za mduara kwa mbali kwenye ngoma hiyo.
Darasa amefunguka kwenye kipindi cha ‘The Jump Off’ cha 100.5 Times
fm alipokuwa akiutambulisha wimbo wake, ambapo Jabir Saleh aka Kuvichaka
alitaka kufahamu ngoma hiyo ni aina gani ya hip hop.
“Kwenye maisha hauwezi kuwa serious muda wote, sasa huu ndio muda
wangu wa kutania na ndio maana nacheza na ndio maana nimeweka kwenye
mixtape. Nikiwa serious narudi darasani na tunafanya mambo yetu yale.”
Alifunguka Darasa.
Alipoulizwa kuhusu lengo lake la kuwakutanisha Shilole kwenye ngoma
hiy, mkali huyo wa ‘Weka Ngoma’ alifunguka, “Nilikuwa nataka tofauti, as
you can see umeona tofauti. Na tofauti niliyokuwa mimi, kwanza nilikuwa
nachukua mashabiki wa Shilole na mashabiki wangu nawaweka kwenye chumba
kimoja.
“Tunatengeneza familia kutoka kwa watu ambao tulikuwa hatufahamiani
tunakaa chumba kimoja, marafiki wangu mimi na marafiki wa Shilole na
Mchizi Mox sasa hivi wamekaa chumba kimoja wanatusikiliza.” Darasa
alifafanua.
No comments:
Post a Comment