Exclusive: Linex kusaini mkataba na kampuni itakayosimamia muziki na ratiba ya maisha yake binafsi, 'sitaki u-manager wa kuombana hela'
rap stars
Mwimbaji wa ‘Kimugina’ Linex anatarajia kusaini mkataba na
kampuni inayoendeshwa na vijana wa hapa Tanzania itakayosimamia kazi
zake za muziki, lakini tofauti na management nyingi za Kibongo kampuni
hiyo itasimamia hadi ratiba zake binafsi ikiwa ni pamoja na mitoko ya
kawaida.
Linex ameiambia tovuti ya Times fm kuwa kwa muda wa miaka minne
amekuwa akifanya kazi bila kuwa chini ya management yoyote kwa kuwa
alikuwa hajapata manager anaemfaa.
“Unajua kuna point Artist unafika unakuwa hauwezi kuendesha kila kitu
mwenyewe. Mimi nimeweza kuendesha muziki wangu bila kuwa na manager, na
kitu kilichokuwa kina sababisha mimi nashindwa kuwa na management ni
kwa sababu nilikuwa sitaki kuwa na manager ambaye mimi nakuwa namuomba
pesa. Sikutaka kuwa na manager ambaye sijui namuomba pesa ya kufanya
video. Nilitaka manager ambaye mimi napokuwa na njaa na yeye anakuwa na
njaa, ndo manager ninayemtaka.
Manager ambaye anajua Linex sasa hivi afanye nini, sehemu gani ambako
ana soko anaweza kufanya biashara, ni sehemu gani ambayo Linex amefeli
inabidi tupambane afanye wimbo mpya na ni audience wa aina gani Linex
anawakosa. Huyo ndiye manager niliyekuwa namtaka.” Amesema Linex.
Msanii huyo anayeuwakilisha vyema mkoa wa Kigoma amesema leo ndio
siku ambayo watakaa na kampuni hiyo kwa ajili ya kumalizia maongezi yao
waliyoyaanza jana ikiwa ni pamoja na kile ambacho anakitaka yeye, kuwa
na manager ambaye sio tu ataangalia muziki wake bali atacontrol ratiba
binafsi ya maisha yake.
“Tulikuwa kwenye kikao jana na tumezungumza mambo mengi, kiasi kwamba
tunachokisubiria sasa hivi ni kwamba natakiwa mimi nikae niandike rules
zangu, yaani kwamba mimi nataka kufanya vipi kazi na hiyo kampuni. Na
wao wataniambia kwenye hizo rules zangu ni zipi zinatakiwa ziwepo na
zipi zinatakiwa zitoke.
“Yaani nataka kuwa na management ambayo ina-control hadi maisha yangu
ya kawaida. Labda kwa mfano, Linex mwezi huu labda ulitoka ulienda
sehemu flani, mwezi unaokuja wewe hutakiwi kwenda sehemu yoyote kwa
sababu kuna biashara hii na hii kwa hiyo hutakiwi kutoka. Yaani niwe mtu
wa studio, nimeenda gym nikitoka narudi nyumbani basi.”Amefunguka
Linex.
‘Mama Halima hit Maker’ anataka hata mitoko yake ya kula bata kawaida
iwe chini ya usimamizi maalum, “Hadi kutoka kwangu sio kwenda labda
wapi wapi, nataka kwenda sehemu sijui kwa sababu mimi ni binadamu nataka
ku-enjoy. Lakini nataka watu ambao wanaweza ku-control hadi maisha
yangu. Sitaki manager miyeyusho, u-manager wa kuombana hela..na ndio
maana nilipambana mwenyewe.”Amesema Linex.
Utamsikia kwa urefu Linex kwenye 'Bongo Dot Home' ya 100.5 Times fm, Jumamosi (November 16).
No comments:
Post a Comment