Tuesday, October 29, 2013

Ben Pol aeleza kilichomsukuma afanye video ya Jikubali na Nisher

rap stars
Ben Pol aeleza kilichomsukuma afanye video ya Jikubali na Nisher

Ben Pol amesema aliamua kumpa Nisher kazi ya kuongoza video yake ya Jikubali kwakuwa alifahamu ni mtu aliyekuwa na hasira ya kuonesha uwezo wake.

"Kikubwa niliona ni mtu ambaye ana moto, unajua mtu anapokuwa ameanza halafu ana moto obvious anataka kufanya vitu vizuri vikubwa yaani damu inachemka unaweza kusema anatafuta  exposure pia," amesema Ben Pol

"Kwahiyo nilimpa kwa sababu hizo, kwa sababu niliona yeye kazi zake za mwanzo alizozifanya za akina MABESTE za akina nani ni kazi kali sana. Anafanya kwa nguvu sana  na ubora wa hali ya juu.

Kwahiyo nikaona huyu mtu akipata audio nzuri anaweza kufanya kitu kikubwa  ndio maana nikafikiria kumpa. Nikaona bado ni mpya, bado ana njaa, bado ana ubunifu mwingi, unajua tofauti na ukimpa director ambaye ameridhika ana miaka mitano, kumi katika industry anaweza akakufanyia kama moja ya kazi zake za kila siku kwa hiyo mimi nilikuwa naiepuka. Kwahiyo mimi nilikuwa nataka kama mtu unampa kazi afanye kazi hiyo hiyo pekee yake."

No comments:

Post a Comment