Tuesday, October 29, 2013

Vanessa Mdee afanya collabo na Iyanya wa Naija





Siku hizi kila msanii mkubwa anayekutana na msanii mkubwa huwaza kufanya makubwa. Cha kwanza ni kubadilishana contacts na kuongea lugha ya muziki, collabo.

Baada ya Diamond Platnumz kufanya remix ya 'My Number One' na ‘Davido’ wa Nigeria aliyekutana naye Dar, huenda msanii wa B’Hitz, Vanessa Mdee aka Vee Money akawa na wazo la kufanya collabo na mkali wa ‘Kukere’ Iyanya wa Naija.
Hisia hizo zinakuja baada ya Vee Money kupost kwenye Instagram picha akiwa na Iyanya.
Japo hakuandika kilichozungumzwa kati yao lakini swali aliloliandika kusindikiza picha hiyo, linatoa picha kuwa huenda wawili hao waliongea pia kuhusu kufanya kazi siku moja.
Ama huenda tayari wimbo ukawa jikoni? Who knows?
“Could there be a song in the making? #It’sIYANYA #EastMeetsWest @iyanya,” ameandika Vanessa kwenye picha hiyo.
Kama ndivyo, basi collabo za Watanzania na Wanaijeria zikawa nyingi siku za usoni. Tunangojea kwa hamu kubwa.
rap stars

No comments:

Post a Comment