Msanii Kanye West ajitamba na kuweka wazi kuwa yeye ndiye msanii
namba moja duniani wa miondoko ya ‘Rock’, hayo aliyasema katika moja ya
mahojiano yake aliyoyafanya kwenye kituo kimoja cha redio cha Uingereza.
Rapa huyo aliweka wazi kuwa yeye ni miongoni wa wanamapinduzi katia
muziki huo huku akisisitiza kuwa asingekuwepo yeye kama Michael Jackson
asingekuwepo.
Alienda mbali zaidi baada ya kuweka wazi kuwa ndani ya miaka 10
ameweza kupiga hatua kubwa kama mbunifu na mtu maarufu, pia aliweza
kumsifia rafiki yake wa karibu Jay Z, kwa hatua aliyofikia na kudai kuwa
yupo juu zaidi yake.
No comments:
Post a Comment