Tuesday, October 29, 2013

Exclusive: Izzo Bizness asema ataufunga mwaka na 'Inanichosha', awapa shavu Jay Moe, Fid Q na Shaa, agusia vinavyomchosha

rap stars


Rapper mjasiriamali toka Mbeya Izzo Bizness amejipanga kuufunga mwaka huu kwa collabo nzito inayoitwa ‘Inanichosha’ iliyoguswa na mikono ya producer mkongwe na mmiliki wa MJ records, Joachim Kimario aka Master Jay.
Akiongea na tovuti ya Times fm, Izzo B amesema amewashirikisha wakali wa mashairi na flow Fid Q na Jay Moe, na member wa zamani wa Wakilisha, Shaa.
Amesema mdundo wa wimbo huo umetayarishwa na producer KTB wa Mbeya, kisha Vocal na Mixing zimefanywa na Master Jay.
Izzo Bizness amegusia ujumbe uliozungumziwa kwenye wimbo huo,ukiwa unayalenga yale yanayomchosha.
 “Kuna vitu tumeongea tu ambavyo vipo vinaendelea katika maisha, katika hii game ambavyo vinachosha, yaani kwamba habari flani na hali flani inayoendelea inachosha , unajua. Nafikiri ikitoka watu ndo wataelewa nini ambacho namaanisha zaidi kwa sababu utamu hatuwezi kuumaliza sasa hivi.” Amesema Izzo Bizness.
 Ni lini ngoma hiyo itaachiwa rasmi, ‘Ball Player hit maker’ akafunguka, “sijajua bado siku ya kuiachia kwa sababu Master Jay ndo anaimalizia, kwa hiyo ikiwa iko tayari tu nafikiri hata leo ikiwa tayari watu watajua lini naiachia.”
Mkusanyiko wa vichwa hivyo kwenye ‘Inanichosha’ kunaweza kutoa picha ya kitu kikubwa kinachoweza kuwa ndani ya ngoma hiyo. Endelea kufuatilia hapahapa.

No comments:

Post a Comment